Seneta Wafula Wakoli amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha mafunzo ya kilimo cha Mabanga ATC na kusikitishwa na hali duni ya vifaa, ikiwemo matrekta ambayo hayajakarabatiwa kwa zaidi ya miaka miwili.
BY FELIX WANJALA

Mkuu wa kituo hicho, James Musoti, alieleza kuwa taasisi imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa fedha kutoka kwa serikali ya kaunti, na akatoa wito kwa bunge la kaunti kuidhinisha mswada utakaolipa kituo hicho uhuru wa kifedha ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Baadhi ya wafanyakazi walionyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kituo, wakisisitiza kuwa Mabanga kihistoria imekuwa nguzo muhimu kwa wakulima na wanafunzi katika sekta ya kilimo ya eneo hilo.
Seneta Wakoli alitoa wito kwa utawala wa Gavana Kenneth Lusaka kutenga rasilimali zaidi kwa idara ya kilimo na kuidhinisha hatua zitakazoliwezesha kituo hicho kurejesha heshima yake ya zamani na kuhudumia jamii kikamilifu.