

Kwenye Ligi Kuu ya FKF humu nchini, Posta Rangers waligawana pointi na Mara Sugar baada ya kutoka sare ya 1-1 leo alasiri katika Uwanja wa Kenyatta. Posta Rangers walichukua uongozi mapema Machakos baada ya Faustin Ojiambo kufunga goli, akisaidiwa na Curtis Wekesa. Baadaye, kabla ya kipindi cha mapumziko, Raila Christopher alisawazisha kwa Mara Sugar FC kwa kichwa bora, akisaidiwa na Steve Otieno, na kupelekea sare ya 1-1.Katika michezo ya kimataifa, katika ratiba ya marudiano ya UEFA Champions League, Borussia Dortmund itakutana na Sporting Lisbon katika Uwanja wa Signal Iduna Park saa 8:45 usiku , huku Dortmund wakiwa na jumla ya mabao 3-0. Baadaye, saa 11:00 usiku, Paris Saint-Germain itacheza dhidi ya Brest katika Uwanja wa Parc des Princes, huku PSG ikiwa na jumla ya mabao 3-0.
Wakati huo huo, PSV Eindhoven itakutana na Juventus katika Uwanja wa Philips, huku Juventus wakiwa na jumla ya mabao 2-1. Hatimaye, mechi inayosubiriwa na wengi, Real Madrid itachuana na Manchester City katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, huku Real Madrid ikiwa na jumla ya mabao 3-2, iliyofungwa kwenye kipute cha kwanza,hili likimpa kocha mkuu waa man city pep Guardiola kibarua kigumu.