

Kwenye hafla ya mazishi ya mzee kingi mwaruwa babake spika wa bunge la seneti amason kingi,rais William Ruto aliwasuta wapinzani wake aliodai wanaendesha siasa za ubaguzi nchini,rais amesema kila mkenya ana haki ya kupata maendeleo.
Viongozi wa kidini waliohudhuria hafla hiyo ya mazishi waliwarai wakenya kujisajili na bima mpya ya afya ya SHA wakidai imetoa mchango mkubwa kwa wasio na uwezo wa kukimu ada ya matibabu.Rais alitumia fursa hiyo kuwashambulia wale alidai wanapinga ajenda zake kwenye mitandao ya kijamii,ikiwemo ahadi ya ujenzi wa barabara eneo la kaskazini mashariki mwa taifa.Rais William Ruto aliandamana na viongozi mbalimbali kwenda kumfariji spika kingi eneo la magarini kaunti ya kilifi.
