

Huku shinikizo la kuondolewa kwa jaji wa mahakama kuu Martha koome zikishika kasi, aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua na kundi lake wameonekana kupinga hatua hiyo wakidai jamii nzima ya eneo la mlima Kenya inalengwa na serikali.Wandani wa Gachagua walimtaka aungane na kiongozi wa upinzani Raila Odinga,ili kuendelea kuikosoa serikali,hatua ambayo imekuwa ikipingwa na baadhi ya wabunge,wandani wa rais William Ruto.
Hata hivyo viongozi hao waliisuta serikali kwa madai kwamba imefeli kuheshimu ujumbe kutoka kwa viongozi wa makanisa wanapoikosoa serikali kuhusu utendakazi wake.Awali askofu mkuu wa kanisa katoliki kutoka jimbo la nyeri,Antony Muheria,alijipata pabaya baada ya kuwataka viongozi kukoma kusimulia yale wametekelezea wananchi,muheria alipata majibu kutoka kwao.Aidha Gachagua aliyehudhuria ibada ya jumapili eneo la igmbe kaskazini kaunti ya meru,aliwarai viongozi wa eneo hilo,kujiunga na chama chake kipya anachopania kuzindua mei mwaka huu.