

Pendekezo la kubuniwa kwa wadhifa wa waziri mkuu,umepingwa na baadhi ya wakenya, ambao wamemtaka kiongozi wa upinzani Raila Odinga,kupuuza pendekezo hilo, wananchi hao wameshabikia hatua ya kiongozi huyo,kupoteza kiti cha umoja wa Afrika.Wametoa wito kwa raila kurejea nchini ili kuendelea kuikosoa serikali, huku wakidai kwa sasa upinzani umelemazwa.Baadhi wamemtaka waziri huyo mkuu wa zamani kushirikiana na viongozi wengine wa upinzani,ili kubuni muungano utakaomenyana na rais William Ruto katika uchaguzi wa 2027.

Aidha baadhi walikuwa na mtazamo tofauti,ambapo walidai ushirikiano wa rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga,ni wa kuleta umoja wa taifa.Hata hivyo kabla ya kutunukiwa wadhifa wa Waziri Mkuu nchini Kenya, hatua kadhaa zinahitajika, kulingana na katiba ya sasa Kenya haitambui wadhifa wa Waziri Mkuu.” Wadhifa huu uliondolewa baada ya Katiba ya 2010 kuanza kutumika, wadhifa huu ulitumika wa makubaliano ya serikali ya nusu mkate kati ya 2008 na 2013.
Wakati huo, wadhifa wa Waziri Mkuu ulipewa kiongozi wa chama au muungano wenye idadi kubwa ya wabunge bungeni.Ili kuwepo na wadhifa huo kwa sasa,katiba itahitajika marekebisho ili kurejesha wadhifa huo, Marekebisho hayo yatatakiwa kupitishwa bungeni na idadi kubwa ya wabunge. Na je majukumu ya waziri mkuu ni uepi, mwanzo,utahusisha kuongoza serikali, kusimamia baraza la mawaziri, na kufanya kazi kwa karibu na Rais, kulingana na jinsi wadhifa huo utakavyobainishwa katika mfumo mpya wa kikatiba.Kwa sasa rais ndiye mwenye madaraka makuu nchini.