

BY EMMANUEL WABOMBA, TMG JOURNALIST.
𝗠𝗮𝘀𝗵𝗶𝗻𝗱𝗮𝗻𝗼 𝘆𝗮 𝗠𝗽𝗶𝗿𝗮 𝘄𝗮 𝗪𝗮𝘃𝘂 𝘆𝗮 𝗗𝗮𝗻 𝗪𝗮𝗻𝘆𝗮𝗺𝗮 𝗔𝗺𝗯𝗼𝘀𝗲𝗹𝗶 – 𝗞𝗹𝗮𝗯𝘂 𝘆𝗮 𝗪𝗮𝗻𝗮𝘂𝗺𝗲 𝘆𝗮 𝗕𝗼𝗸𝗼𝗹𝗶 𝗻𝗮 𝗦𝗵𝘂𝗹𝗲 𝘆𝗮 𝗨𝗽𝗶𝗹𝗶 𝘆𝗮 𝗪𝗮𝘀𝗶𝗰𝗵𝗮𝗻𝗮 𝘆𝗮 𝗞𝗲𝘀𝗼𝗴𝗼𝗻 𝗬𝗮𝗻𝗴’𝗮𝗿𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗨𝘀𝗵𝗶𝗻𝗱𝗶 𝘄𝗮 𝗨𝗯𝗶𝗻𝗴𝘄𝗮.
Mashindano ya Dan Wanyama ‘Amboseli Volleyball Tournament’ yamekamilika kwa kishindo huku Klabu ya Wanaume ya Bokoli na Shule ya Upili ya Wasichana ya Kesogon wakitwaa mataji ya ubingwa.Fainali hizo zilifanyika katika uwanja wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Bokoli, Kaunti ya Bungoma, na ziliwavutia maelfu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia ushindani wa hali ya juu.
Katika kitengo cha wanaume, Bokoli walidhihirisha umahiri wao kwa kuwashinda Kakamega Kings kwa seti 3-1. Seti ya kwanza ilishuhudia Bokoli wakishinda kwa alama 25-20, kabla ya Kakamega Kings kurejea kwa ushindi wa 21-25 katika seti ya pili. Hata hivyo, Bokoli walionyesha uthabiti na kushinda seti ya tatu na ya nne kwa alama 25-18 na 25-16 mtawalia, na hivyo kutawazwa mabingwa.Kwa upande wa wanawake, Shule ya Upili ya Kesogon kutoka West Pokot waliandika historia kwa kuwashinda Bishop Sulumeti kwa seti 3-2 katika mechi iliyosheheni msisimko na kasi ya hali ya juu.Safari ya mafanikio ya timu hizi haikuwa rahisi.

Bokoli walifuzu fainali kwa ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Bungoma Mseto, huku Kakamega Kings wakipata tiketi ya fainali baada ya kuwashinda Merewet ya Uasin Gishu kwa seti 3-0. Kwa upande wa wanawake, Kesogon walifanikiwa kuwashinda Lugulu Girls kwa seti 3-1, hali sawa na Bishop Sulumeti walipowafunga Kosirai kutoka Nandi.Mashindano haya, ambayo yalihusisha shule za sekondari, vyuo, na hata sekondari ya awali, yameibua vipaji na kuonyesha ukuaji wa michezo nchini. Mheshimiwa Dan Wanyama, mfadhili wa mashindano haya, aliwahimiza wachezaji kudumisha nidhamu kama msingi wa kukuza vipaji vyao.Pia alibainisha kuwa serikali imejizatiti kuboresha viwango