
Rais wa Kenya William Ruto akitoa matamshi yake wakati wa mkutano wa pamoja na wanahabari katika hotuba ya hafla iliyopita

FELIX WANJALA.
Baadhi ya wakaazi wameelezea matumaini yao kuwa Rais William Ruto atatekeleza ahadi aliyoitoa hivi karibuni ya kuchangia kwenye bima mpya ya afya ya SHA, ili kusaidia Wakenya wasiokuwa na uwezo kumudu huduma za afya.
Wakizungumza na wanahabari, wakaazi hao waliongeza kuwa mchango wa viongozi wakuu, wakiwemo wabunge na magavana, utakuwa mfano bora wa uongozi wa kuwajali wananchi wa kawaida.
Aidha, wananchi wengine wamepongeza hatua zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na vitendo vya ufisadi katika sekta ya afya. Wanatumaini kuwa juhudi hizo zitaimarisha uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Wakati huo huo, baadhi ya wananchi wamewataka Wakenya kumruhusu Rais Ruto kuendelea kutekeleza ajenda yake, wakisema bado ana takribani miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027 – muda wanaoamini unatosha kuona mabadiliko chanya.

Katika kikao na viongozi wa kaunti ya Turkana, Rais Ruto alitangaza kuwa atachangia wakenya1.5 kwa ajili ya bima ya afya, na akatoa wito kwa wabunge na magavana kuungana naye kwa kuchangia kwa hiari ili kuwasaidia maelfu ya Wakenya wasiojiweza.