
BY FELIX WANJALA
Usimamizi wa makao makuu ya kimikakati ya Eninga,Leo imetoa taarifa kwenye vyombo vya habari,na kulaani vikali tukio la jumamosi asubuhi, ambapo wahuni walivamia eneo Hilo, na kusababisha uharibifu wa mali,pamoja na kuwajeruhi baadhi ya wafanyikazi na walinzi,wa mgombea wa ugavana Bungoma Timothy Wanyonyi.Akizungumza na wanahabari, meneja wa kampeni ya mgombea huyo, Erick Makokha,amewaonya wapinzani wa Wanyoyi, dhidi ya kuendelea kufanya siasa za migawanyiko,akidai Haina nafasi katika Kaunti ya Bungoma.
Alikiri kuwa licha ya uvamizi huo,mgombea huyo amejitolea kuhakikisha, anaipa elimu kipao mbele kwa kufdadhili masomo ya wanafunzi wasiojiweza katika jamii,wa Gredi ya kumi,wa shule za upili,zile za kiufundi na vyuo vikuu. Kuendeleza masomo yao pasipo na ugumu wowote.
Makao ya Eninga ilikiri pia itasimama na familia zote zenye mziba,pia iliahidi kuunga mkono michezo ili kukuza talanta,ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa vifaa hitajija.Kwenye sekta ya afya mgombea huyo ana mpango wa kufanikisha bima ya Tim care itakayowezesha wakaazi wa Bungoma kupata matibabu Bora na ya bei nafuu,ameahidi kuanzisha mpango wa Linda mama kwa akina mama wote watakaojifungua,kwamba serikali ya Kaunti itagharamia matibabu.
Katika tukio la jumamosi wamesema watatoa ushahidi wote unaohitajika kwa vitengo vya usalama ili kurahisisha uchunguzi.Wamewataka polisi kuhahakisha uchunguzi na watakaopatikana kuhusika kwa uvamizi huo wachukuliwe hatua kali za kisheria.