Kenya inaendelea kukumbwa na changamoto za ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, gharama kubwa ya maisha, na madai ya uongozi mbaya na ufisadi. Hali hii imeibua hisia kali za wananchi kuhusu serikali na taasisi zake. Picha hii imezalishwa na AI kwa maelezo mafupi PEKEE/
FELIX WANJALA

Kenya inaendelea kukumbwa na changamoto za ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, gharama kubwa ya maisha, na madai ya uongozi mbaya na ufisadi. Hali hii imeibua hisia kali za wananchi kuhusu serikali na taasisi zake.Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la Tiifa mwaka 2026, asilimia 68 ya Wakenya hawana imani na Rais William Ruto, huku 29% pekee wakionekana kuamini uongozi wake. Aidha, jumla ya uaminifu kwa rais imesalia katika kiwango hasi cha -39%.
Mashirika mengine ya serikali pia yamekumbwa na ukosefu wa imani. Asilimia 72 ya wananchi hawana imani na Bunge, 69% hawana imani na polisi, 68% hawana imani na vyama vya kisiasa, na 67% hawana imani na serikali za kaunti. Tume ya uchaguzi (IEBC) imepoteza imani ya 66% ya wananchi miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu, huku 60% wakikosa kuamini idara ya mahakama.
Katika sekta ya uchumi, 64% ya Wakenya wanaamini hali imezorota chini ya uongozi wa Rais Ruto, huku 19% pekee wakiona uchumi umeimarika. Changamoto kubwa zinazotajwa na wananchi ni mfumuko wa bei na ushuru mkubwa (47%), ukosefu wa ajira na umaskini (23%).
Kwa jumla, 74% ya Wakenya wanaamini taifa liko katika mwelekeo mbaya, huku 14% pekee wakiona linaelekea katika mwelekeo sahihi.