Bumula MP Jack Wamboka/HANDOUT
BY FELIX WANJALA

Wafwasi wa Mbunge wa Bumula Jack Wamboka na aliyekuwa mbunge wa zamani Mwambu Mabonga, wametofautiana kuhusu ni nani ndiye kigogo wa kisiasa wa eneo Hilo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ujao.Kauli za Tutam zilionekana kuteka anga huku baadhi ya wafwasi wakionekana kusifia siasa za mwambu Mabonga anayetafutia rais William Ruto uungwaji mkono kuchaguliwa kwa mhula wa pili.
Hatua hii inajiri siku chache baada ya kiongozi wa chama Cha Ford Kenya na spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula kutangaza kuwania urais mwaka wa 2032,imeonekana kubadili kwa kiasi nia ya baadhi ya wakaazi wa eneo hilo ambao wameanza kuishabikia serikali.
Hata hivyo eneo la Magharibi siku za hivi karibuni limekuwa mwenyeji wa viongozi wakuu serikalini wakiongozwa na Msaidizi wa Rais farouk Kibet,Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka mwenzake wa kakamega Fernandez Barasa ,seneta Wafula Wakoli mbunge wa zamani Mwambu Mabonga na Spika Wetangula wakiwarai wakaazi kumpigia kura rais Ruto katika uchaguzi mkuu ujao.
Ubabe wa mwambu Mabonga eneobunge la Bumula umeonekana kuwa tishio kwa mbunge wa Sasa Jack Wamboka ambaye anajihusisha na seneta wa Nairobi Edwin Sifuna katika harakati za kuwarai wananchi wa jamii ya Mulembe kupuzilia mbali uongozi wa Kenya kwanza.