Beki wa Manchester United Harry Maguire ambaye amekuwa nahodha wa timu hiyo kwa Zaidi ya miaka mitatu amedhibitisha kupokonywa kitambaa cha unahodha katika mabadiliko mapya ambayo yanafanywa na kocha mkuu Erik Ten Hag.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Maguire alisema kwamba japo alipokea taarifa hizo kwa kusikitika mno, lakini ndio hivyo maamuzi yameshafanywa ka kusema kwamba ataendelea kutia juhudi zake ili kuipigania nembo ya Manchester United.
“Baada ya mazungumzo na meneja leo ameniarifu anabadilisha nahodha. Alinieleza sababu zake na ingawa mimi binafsi nimekatishwa tamaa sana, nitaendelea kujitolea kila ninapovaa shati. Kwa hivyo nilitaka kusema asante sana kwa mashabiki wa Manchester United kwa sapoti yao nzuri wakati nimekuwa nikivaa kitambaa”Maguire aliandika
Maguire alipokezwa unahodha miaka mitatu na nusu iliyopita na aliyekuwa kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer na amekuwa akipokea kashfa nyingi na masimango kutoka kwa mashabiki haswa kutokana na makosa yake mengi ambayo anafanya uwanjani – makosa ambayo husababisha United kufungwa na wengi wanahisi kwamba ni makosa yanayoweza kuepukika.
Maguire alimshukuru Solskjaer kwa kumuaminia na unadhodha wa timu hiyo yenye historia ndefu, na kudokeza kwamba licha ya kuwepo kwa tetesi za kupoteza matumaini katika kikosi cha kwanza cha United, bado atazidi kujitolea kwa hali na mali kuitumikia timu hiyo.
Kwingineko,Sakata ya uhamisho wa Romelu Lukaku inaonekana kuchukua hatua nyingine kwani ameghairi uhamisho wa kwenda Inter Milan kwa wapinzani wao Juventus msimu huu wa joto.
Mshambulizi huyo wa Chelsea amekuwa na wakati mgumu katika miaka ya hivi majuzi, licha ya kurejea katika kiwango chake bora zaidi kwa Nerazzurri miaka michache iliyopita. Kipindi hicho kilimfanya arudi Stamford Bridge kwa dili la thamani ya pauni milioni 100 tu, akiwa na matumaini ya kuvunja matatizo ya ufungaji wa timu hiyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alifurahia kipindi cha kwanza cha kampeni chini ya Thomas Tuchel, lakini mchanganyiko wa wasiwasi wa jeraha na kisha mahojiano na Sky Italia yalisababisha matatizo wakati wake na The Blues. Lukaku alisema nia yake ya kuichezea Inter kwa mara nyingine tena wakati wa ubora wake, jambo ambalo lilivuruga vyama kadhaa.
Kipindi cha pili cha kampeni kilimshuhudia hasa akitokea benchi, kabla ya hapo kuthibitisha kuondoka San Siro kwa mkopo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa na wakati mseto katika klabu yake ya zamani, huku dalili zote zikielekeza kwenye uwezekano wa kurejea kwenye mkataba wa kudumu msimu huu wa joto.