Machafuko na uhalifu wa aina yake vikiwemo vifo,wizi na ukiukaji wa haki za kibinadamu pamoja na
kupotoka kimaadili ndio matokeo yaliyoshamiri maandamano yaloyotarajiwa kuwa ya amani,lengo lake
kuu likiwa ni kushinikiza serikali kupinda mgongo kumskiza mkenya mwenye malalamishi si
haba.Mojawapo ya malalamishi ikiwa ni gharama ya juu ya maisha.
Kulingana na ripoti ya IPOA,takriban watu 30 wamepoteza maisha yao tangu wingu la kwanza la
maandamano ya Azimio.Majeraha na uharibifu wa mali ni baadhi tu ya maudhi yanayoashiria
maandamano hayo yametiwa doa na hulka za waandamanaji.Maswala yanaibuka ikiwa hawa mama
Mboga na bodaboda wanaotetewa ndio wanaondamana barabarani.Ni ikiwa ni hivyo,waandamanaji
hawa wenye kulilia ushuru wa juu na ughali wa maisha wanaweza kugeuka na kuwa wahalifu kiwango
hiki?
Ikiwa sivyo,mama mboga na bodaboda wanapofunga biashara yao kwa sababu ya maandamano,wao
huenda wapi?Mbona wasijumuike kwenye maandamano?Kumeshuhudiwa sehemu kadhaa
waandamanaji wakiwalemea maafisa wa polisi waliolazimika kutumia nguvu kupita kiasi
kujitetea.Maandamano ya sasa yanaonekama kugeuka na kuwa vita kati ya maafisa wa polisi na
wananchi
Baada ya maandamano ya Ijumaa,imebainika kuwa serikali imejitenga na maandamano ya Azimio na
kupuuza Azimio wakiwalinganisha kama wahalifu wanaopania kutatiza shughuli za serikali.
Katika ujumbe wake kwenye Twita,Makau Mutua anayekisiwa kuwa msemaji wa kinara wa Azimio
aliandika,njia mwafaka ya kusuluhisha matataiza ya Wakenya ni kupitia tu kwa mazungumzo .Hii
inachora taswira kuwa huenda Azimio wanataka kuketi meza moja ya Mazungumzo na rais,
mazungumzo yao yakiendeshwa tofauti ikilinganishwa na ya le ya Mazungumzo ya maridhiano.Serikali
nayo imeonekana kukana mazungumzo yeyote tofauti na yale ya Kamati ya wanachama 14. We
Ni hatua gani watakayochukua Azimio kuafikia nia zao pasi ni kusababisha uhalifu barabarani.Serikali
ishughulikie vipi maisha ya wakenya millioni hamsini ikiwa ilishindwa kuwalinda wakenya thelathini
ambao wameangamia kwa mtutu,mali zikiharibiwa.Mswada wa fedha uliositishwa kotini sasa ni hatari
inayoikodolea serikali macho ikiwa mswada huo wanaosema una manufaa utatupiliwa mbali kwani ndio
unaotegemwa sana na bajeti ya serikali.Serikali itafanyaje?
Related Stories
October 27, 2023
October 26, 2023
October 26, 2023