Oktoba 15, Kila mwaka husherehekewa kama siku ya Kuisha mikono ulimwenguni.Siku huhusisha
kampeni tofauti kama kuwapa ufahamu watu kwa umuhimu wa kuosha mikono kwa maji safi na
kutumia sabuni. Mafunzo kuhusu umuhimu wa kudumisha afya bora na kuzuia uchafu wa vyakula.
Kipaumbele ya siku hii ni mikono safi kwa wote ,ila ya mwaka huu 2023 ni ukaribu wa mikono safi. Katika
hafla hiyo siku ya jumapili ilisisitizwa kuwa kupitia uongozi imara na jitihada za pamoja ,tunaweza kufikia
mazoea ya mikono safi kwa wote na ni jukumu la Kila mtu kuhakikisha usafi wa mikono.
Akizungumza katika hafla hii mkurugenzi wa huduma za kinga Daktari Carol Ngunu alisema kuwa
takriban asilimia hamsini ya magonjwa na pia asimia hamsini ya vifo vinaweza kuounguzwa kwa kuosha
mikono mara kwa mara .
Wadau mbalimbali wa afya walitoa wito kwa wakenya kuzingatia kuosha mikono kabla na baada kula na
pia baada ya kutumia vyumba vya kujisaidia, kwa kufanya hivi wanapunguza uwezekano wa kupata
magonjwa kama ya kuendesha na yale yanayosababishwa na virusi ama bacteria.
Waliahidi kuendesha kampeni za muda wa majuma mawili ,ambazo zitalenga kuwapa mafunzo wakenya
waliosehemu zinazopitia changamoto mfano wakazi katika nyumba za kimsingi, mahali pa mikusanyiko
kama makanisa na pale pa watoto wasio na ufahamu zaidi kuhusu umuhimu wa kuosha mikono kama
kwenye shule.
Kulingana na takwimu za kutoka wizara ya afya mwaka wa 2022 kuhusu uwepo wa vifaa vya kunawa
katika kaunti mbalimbali, kaunti ya Nairobi iliibuka ya kwanza kwa asilimia tisini na tatu 93%, huku
ikifuatwa na kaunti ya Kajiado kwa asilimia themanini na sita 86% hata hivyo, kaunti za Tana river na
Wajir zilisalia nyuma kwa asilimia Saba 7% sawia.
Idara ya afya katika kaunti ya Nairobi imeweka matayarisho ya kuhakikisha usalama wa maji hasa katika
kipindi hiki mvua za El nino ambazo zinatarajiwa mwezi huu.Wanaafya walivitaka vituo vyote vya afya
vilivyoteuliwa kwa minajili ya kushughulikia dharura zozote zinazoweza kutokea wakati wa mvua hizi,
ziwe tayari kufanya kazi.
Nicholas Bwire Wandera ambaye ni mkazi wa Bungoma aliishukuru serikali kwa matayarisho iliyoweka
,hasa serikali kuu, katika kipindi hiki cha El nino ,aliendelea kuomba wizara ya afya kuendelea kusisitiza
usafi katika kipindi hiki kwani magonjwa mengi hupatikana wakati kama huu wa masika na mafuriko.
Abigaely Wanjala