‘FATAL BETRAYALS’
Sanaa ya uigizaji nchini umekuwa kitega uchumi hasa miongoni mwa vijana nchini,
Ignetius Nyukuri Mwigizaji mkuu katika filamu hii anasema serikali ya kaunti na kitaifa inafaa kutambua sanaa ya usanii nchini pamoja na kuipa kipao mbele kama vile wanavyofanya katika maswala ya afya na ujenzi wa miundo musingi.
Wanawake wanahitajika kupewa nafasi ya kuonyesha talanta zao katika tansia ya uigizaji,mwandishi wa filamu ya Fatal Betrayals amewataka akina dada kujitokeza ili talanta zao ziweze kutambuliwa ,Dotty Akinyi anasema kuna changamoto kadhaa wanapitia kama waigizaji wa kike nchini.
Mwelekezi mkuu katika maswala ya fasheni Timoth Trevor anasema katika tansia ya usanii, Umoja,kutokata tamaa na kujiamini ndizo nguzo kuu msanii yeyote anafaa kuzingatia wakati wa uigizaji.
Fatal Betrayal ni filamu iliyoandikwa na Dotty Akinyi akishirikiana na Austine Kwatera, Austine anasema filamu ni mradi unaoweza kumgharimu mtu kiasi kikubwa cha pesa ili kufanikishwa.
Filamu hii itazinduliwa tarehe 28 oktoba mwaka huu katika eneo la wanangali kaunti ya Bungoma,Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo.
FELIX WANJALA