Christiano Ronaldo, Bruno Fernandez na João Felix waliwaweka Portugal kileleni Kwa kufunga mabao.Portugal wanaongoza kwenye kundi J katika mechi za Euro 2024 .
Walipata ushindi wa mabao manne dhidi ya Bosnia.Ronaldo ameendeleza kampeni ya kufunga.
Matokeo mengine ya hapo jana ni kama yafuatavyo:
Ubelgiji na Uswidi walipata alama moja.
Ugiriki nao wakapoteza dhidi ya Netherlands.
Austria wakapata ushindi wa bao moja dhidi ya Azerbaijan.
Hayo yakijiri, Kenya na Russia walitoka sare ya mabao mawili kule Antalya.Masoud Juma na Akumu ndio wafungaji wa timu ya Kenya.Russia nao walipata bao la pili muda ukiyoyoma.
Matokeo ya mechi sawia na hizi ni kama yafuatavyo:
Senegal walishinda dhidi ya Cameroon.
Misri na Algeria walitoka sare ya moja.
Nigeria nao wakashinda dhidi ya Mozambique.
Baada ya kucheza na Russia,Kenya watawaalika Croatia Kwa mechi nyingine ya kirafiki.
Na Michael Simiyu