Akizungumza wakati wa kikao cha vijana uongozini kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga ameitaka serikali kuu kubainisha majukumu yaliyogatuliwa na ya kitaifa, Odinga Amesema ni lazima serikali kuu iondoe vikwazo dhidi ya miradi ya serikali za kaunti.
Odinga sasa anadai mamlaka mbalimbali za ujenzi wa miundo msingi nchini,ikiwemo barabara amesema mamlaka hizo zimekuwa vikwazo kubwa kwa serikali za kaunti,katika ujenzi wa barabara, mamlaka hizo ni KERA,KENHA na KURA.
Raila ameitaka serikali kufutilia mbali mamlaka hizo akisema majukumu yake yamechukuliwa na serikali za kaunti.Odinga amefafanua kuhusu swala la ujenzi wa nyumba za bei nafuu,maeneo ya viwanda na masoko ya kisasa,ambayo ametaka pia kuachiwa serikali za kaunti.
Kiongozi huyo wa upinzani amesema hatua ya serikali ya kitaifa kukwamilia majukumu ya kaunti ni njia mojawapo ya wizara hizo kuendeleza ufisadi,amemtaka rais William Ruto kuwa mstari wa mbele kushughulikia swala hilo.
Serikali ya Rais William Ruto imeonekana kufanikisha mpango wa kutambua afya ya jamii,Raila ameonekana kupinga hatua hiyo ya serikali,Mjadala huo wa kuhusu majukumu yaliyogatuliwa ambayo mengine yamesalia chini ya serikali kuu ambayo yalipewa kipao mbele wakati wa kongamano la ugatuzi lililoandaliwa mwaka huu kaunti ya Uasingishu.
Na Felix Wanjala