
Marcus Rashford na Harry Kane waliwaweka Uingereza kileleni Kwa kufunga mabao ya ushindi.Harry Kane akifunga mabao mawili,moja ikiwa penalti iliyosababishwa na Jude Bellingham.Uiengereza wamefuzu Kwa awamu nyingine ya Euro 2024.

Mudryk naye aliwaweka kileleni Ukraine Kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya Malta.Alikuwa na nafasi nyingi alizoshindwa kukamilisha.Ukraine walishinda mabao matatu dhidi ya Malta.
Serbia walishinda dhidi ya Montenegro Kwa mabao matatu.San Marino wakapoteza dhidi ya Denmark.Lithuania na Hungary wakatoka sare ya mabao mawili.Slovenia nao wakashinda dhidi ya Ireland Kaskani.
Mechi za usiku wa leo ni kama zifuatazo:
Wales wako ugenini dhidi ya Armenia.Netherlands ni wenyeji wa Ireland.Uswizi watawaalika Kosovo na mwishowe Croatia watakuwa wageni Kwa Latvia.
Baada ya Euro 2024,ligi kuu ya Uingereza inarejea wikendi hii.
Na Michael Simiyu