Baadhi ya wachezaji wa timu ya Chelsea wamerejea klabuni humo baada ya mechi za kimataifa.Chelsea wanajiandaa Kwa mchuano mkali dhidi ya Asenali wikendi hii. Nahodha wa Chelsea Reece James amerejea kwenye mazoezi baada ya kuuguza majeraha msimu ulipoanza . Anatumai kusakati dhidi ya Asenali. Moses Caicedo na Enzo Fernandez wapi njiani kurejea uingereza.
Kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino anasema yupo tayari kumualika Mikel Arteta uwanjani Stamford bridge.
Huku ligi hio ikirejea ,mechi kadhaa zitachezwa kando na hii zikiwemo;
Liverpool dhidi ya Everton
Manchester city dhidi ya Brighton
Sheffield United dhidi ya Manchester United na mwishowe Newcastle dhidi ya Crystal palace.
Asenali nao wanajiandaa vilivyo dhidi ya Chelsea.Bukayo Saka na Jurian Timber watakua kwenye mechi hio baada ya kuuguza majeraha.Mara ya mwisho Asenali na Chelsea kukutana,The Gunners walipata ushindi wa mabao matatu dhidi ya Chelsea.
Huku ligi kuu ya Uingereza ikingoa nanga,ligi ya mabingwa pia inarejea wiki lijalo.
Na Michael Simiyu.