
Champions League logo is seen prior to the Champions League football match between Bologna FC and Borussia Dortmund at Renato Dall'Ara stadium. Bologna (Italy), January 21st, 2025 (Photo by Insidefoto/Mondadori Portfolio via Getty Images)

Tamasha la UEFA Champions League.
Mchuano wa UEFA Champions League unapoendelea kupamba moto, mashabiki wanajiandaa kwa mechi za kusisimua zilizopangwa.Hivi leo tamasha litaanza kwa mechi kati ya Breast dhidi ya PSG saa 2:45 usiku. Baadaye, saa 5:00 usiku, tutashuhudia Manchester City wakipambana na Real Madrid, Sporting dhidi ya Borussia Dortmund, na Juventus dhidi ya PSV Eindhoven.Burudani itaendelea Jumatano, Februari 12, 2025, na mechi kati ya Club Brugge dhidi ya Atalanta saa 2:45 usiku.

Usiku huo huo, Celtic watacheza na Bayern Munich, Monaco watapambana na Benfica, na Feyenoord watashindana na AC Milan, zote saa 5:00 usiku.Awamu ya mtoano imeweka jukwaa kwa mechi kali, ikiwemo pambano la kuvutia kati ya Juventus na PSV Eindhoven, na Manchester City watakutana na Real Madrid.
Timu ishirini na nne zimefuzu kwa raundi ya 16, na hivyo ushindani umepamba moto. Liverpool na Barcelona walikuwa wa kwanza kufuzu, wakifuatiwa na timu kama Inter, Leverkusen, na Lille.Awamu ya mtoano imepangwa kufanyika tarehe 11-12 na 18-19 Februari, 2025, huku mechi za raundi ya 16 zikifuatia tarehe 4-5 na 11-12 Machi, 2025. Kwa bahati mbaya, wachezaji muhimu watakosa mechi kutokana na majeraha au kadi za adhabu, ikiwemo Bremer na Cabal wa Juventus, na Carvajal na Militรฃo wa Real Madrid
Emmanuel Wabomba, Tandao Media Group Sports Journalist.
vclxy8