

Nchini Kenya, Februari kwa ujumla inachukuliwa kuwa mwezi wa uhamasishaji wa afya ya moyo, ikiwiana na mazoea ya kimataifa ya kutumia februari kuongeza ufahamu kuhusu afya ya moyo na mishipa.Ugonjwa wa moyo ni maradhi yanayoushambulia na kuudhoofisha moyo.Moyo ni kiungo kinachosukuma damu katika mwili wa kiumbe hai.Shinikizo la damu au presha mara nyingi huchangia mgonjwa anayeugua kupata ugonjwa wa moyo,kwani moyo hupanuka na kuwa mkubwa na usipotibu presha vizuri huenda ikakusababishia ugonjwa wa moyo.
Kwa watu wazima ugonjwa wa moyo unaweza kusababishwa na jinsi mtu anavyoishi maisha yake ya kila siku.Kwa mfano vyakula ambavyo unakula,kukosa kufanya mazoezi na pia kuwa mnene kupindukia kunaweza kusababisha kupata ugonjwa wa moyo takwimu mbali mbali zikiwemo za shirika la afya ulimwenguni ,WHO, zinaonesha kuwa watoto wengi hufariki kabla ya mwaka mmoja kwa ugonjwa wa moyo bila kugundulika na kupatiwa matibabu ya haraka,na je,ni dalili zipi amabazo unaweza kuziona kwa mtoto anayeugua ugonjwa wa moyo?