

Katika uchaguzi wa kutafuta mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, ushindani mkali ulizuka kati ya wagombea watatu: aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga; Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Djibouti, Yousuf Mahamoud; na mwenzake kutoka Madagascar, Richard James.Kura zilipigwa Jumamosi, tarehe 15 Februari, 2025, jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Katika mchakato wa awali, Raila Odinga aliongoza kwa kura 22, huku Yousuf Mahamoud kutoka Djibouti akijizolea kura 19. Hata hivyo, Mahamoud alimbwaga Odinga katika msururu wa saba, ambapo alipata kura 33 dhidi ya 22 za Odinga.Raila Odinga, kiongozi wa upinzani, alikubali kushindwa kwa mara ya kwanza katika kinyang’ anyiro hicho, na alimpongeza Yousuf Ali Mahamoud kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa tume ya Umoja wa Afrika. Aidha, Raila alisema atarejea nchini Kenya na kuendelea na majukumu yake kama kiongozi wa upinzani, akiahidi kuwa kuna mengi ambayo atatimiza wakati huo.

Rais William Ruto alizungumzia uchaguzi huo kwa mara ya kwanza, na aliungana na viongozi wengine kumpongeza Yousuf Ali Mahamoud kwa ushindi wake.Hata hivyo, baadhi ya wananchi walionyesha kutoridhika na matokeo ya uchaguzi huo.Kushindwa kwa Raila Odinga kulisababisha baadhi ya Wakenya kumhimiza arudi nyumbani ili kuendeleza harakati zake za kupigania haki za wananchi. Wengine walimshauri kujitosa tena katika kinyangโanyiro cha urais mwaka 2027.
Ninamtakia mheshimiwa Raila Odinga kila la heri katika pilkapilka zake za kilasiku
Asante sana kaka kwa kumtakia Kila la heri ๐๐ค