

Mapigano mapya yaliyozuka katika taifa la kidemokrasia ya Congo yamesababisha waasi wa M23 kuuteka mji Bukavu.Kamati ya usalama ya umoja wa Afrika, imewataka waasi hao kuheshimu utawala wa serikali ya nchi hiyo.Katibu wa umoja wa mataifa Antonio Gutierrez,ameitaka umoja wa Afrika (AU)kufanya mazungumzo ya kina na pande zote ili kuleta mwafaka na maelewano ya kudumu DRC.
Waasi wa M23 wamekuwa wakitoa wito kwa wakaazi kuwa watulivu huku wakiahidi kurejesha amani itakayowezesha kuendelea kwa biashara na huduma mbalimbali za kimsingi.Wanajeshi wa DRC waliokuwa wakitoa ulinzi katika mji wa Bukavu,walijisalimisha kwa waasi wa M23 bila ya kushiriki kwa mapigano yoyote.Inadaiwa baadhi ya wakaazi walianza kupora mali kutoka kwenye maduka Mbalimbali,afisi za serikali na hata zile za umoja wa mataifa.Pindi tu M23 ilipoteka mji huo,iliripotiwa kwamba baadhi ya watu wanahofiwa kuuawa kwenye mji wa Bukavu.