

Kwenye michuano ya jumamosi,Sofapaka ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KCB FC huku AFC Leopards ikitwaa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mara Sugar FC. FC Talanta ilishinda Bandari FC kwa mabao 3-2 katika pambano kali na Ulinzi Stars wakapata ushindi finyu wa mabao 2-1 dhidi ya Murangโa Seal.
Kenya Police waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bidco United. Nayo siku ya Jumapili, Gor Mahia na Tusker FC walimaliza bila bao nao Shabana FC na Mathare United FC pia walishindwa kufunga na kutoka sare tasa. Katika msimamo wa ligi kuu nchini Kenya, Kenya Police imepanda hadi kileleni, wakiwa hawajapoteza mechi 13 baada ya kuanza vibaya katika raundi 8 za mwanzo.

Sasa wanaongoza jedwali wakiwa na pointi 41 kutokana na mechi 21. Tusker FC wanawafuata kwa karibu wakiwa na pointi 39 kutokana na mechi 20 nayo Gor Mahia ipo katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 35 kutokana na mechi 20 walizocheza.AFC Leopards na KCB wanamaliza tano bora wakiwa na pointi 33 na 32 mtawalia kila mmoja akiwa amecheza mechi 20.