

Hili lilionekana katika matukio ya hivi karibuni ambapo Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga alishindwa katika uchaguzi wa uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) na kifo cha Mwenyekiti wa zamani wa IEBC, Wafula Chebukati.
Ni jambo la aibu na kusikitisha jinsi baadhi ya Wakenya wanavyokabiliana na huzuni na kushindwa kwa kusherehekea na kucheka.
Badala ya kuomboleza kifo cha Wafula Chebukati, wakili mwenye heshima mwenye umri wa miaka 63 na mwenyekiti wa zamani wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), baadhi ya watu walicheka na kufanya mzaha kuhusu kifo chake kwenye mitandao ya kijamii. Tabia hii ilionyesha upungufu wa maadili kama wanainchi wa taifa tukufu la Kenya.
Baadhi walimfananisha Chebukati na Samuel Kivuitu, mwenyekiti mwingine wa zamani wa IEBC, wakilinganisha muda walioishi baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi. Ulinganisho huu pia haukuwa na heshima na ulionyesha mtazamo wa kutatiza.Awali, Kushindwa kwa Raila katika AU ilikuwa pigo jingine kwa Kenya, lakini ilikutana na mzaha .Jaribio la Raila halikuwa tu kwa ajili yake binafsi bali kwa taifa zima, na matokeo hayo yalionyesha mtazamo mbaya wa baadhi ya Wakenya.

Hatimaye, matokeo haya ya uchaguzi wa AUC na kifo cha Chebukati yanaonyesha kukosa umoja na huruma, ambazo ni muhimu kwa jamii yenye heshima. Kusherehekea kushindwa au kifo cha mtu ni makosa ya kimaadili yanayoharibu maadili tunayopaswa kuyapenda.Hii inaonyesha haja ya heshima zaidi na hata katika kifo. Au labda angekuwepo hayati mzee Bernard Mambo Mbotela angeuliza,je,huu ni ungwana?