
Picha ya mchezaji wa Hoki- kielelezo cha vekta

BY EMMANUEL WABOMBA, TMG JOURNALIST.
Katika Kaunti ya Kisumu, Shule ya Wasichana ya Huma imeandika historia kwa kushinda ubingwa wa magongo kwa mara ya kwanza.Ushindi huu si tu ni fahari kwa timu hiyo bali pia ni kipimo cha juhudi zao na bidii ya wachezaji.Waliwashinda Kisumu Girls kwa bao moja kwa sifuri na sasa wapo kundi A, wakitarajia kushiriki mashindano ya kitaifa Mombasa mwezi Aprili, kisha ya Afrika Mashariki huko Nakuru mwezi Agosti.
Kwa upande mwingine, Shule ya Wavulana ya St. Joseph Nyabondo imeibuka mabingwa wa raga ya Kaunti ya Kisumu baada ya miaka kumi na moja.Timu hii yenye wachezaji 15 kila upande iliwatoa Maseno kwenye nusu fainali kabla ya kuwashinda Otieno Oyoo kwenye fainali.

Wakiwa kundi A pamoja na Kisii, Gekano, na Rapogi, sasa wanajiandaa kwa mashindano ya Nyanza yatakayofanyika Migori.Kwa upande wa Ratiba ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA Lille watakutana na Dortmund saa mbili na dakika arobaini na tano. Baadaye, saa tano usiku, Aston Villa itakutana na Club Brugge, Atletico Madrid watapambana na Real Madrid, na hatimaye Arsenal wataonyeshana makali na PSV Eindhoven.