

BY EMMANUEL WABOMBA,TMG JOURNALIST.
Rais William Ruto ameongoza uzinduzi wa Mpango wa Wakimbizi katika Ikulu mpango huo kwa jina shirika plan unatazamiwa kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali ya humu nchini na kimataifa kutetea maslahi ya wakimbizi wanaokimbia mataifa yao katika ukanda wa Afrika mashariki pamoja na kuwapa hifadhi hadi hali itakapotejea shwari kwenye mataifa yao.
Kwenye mkutano huo rais William Ruto alitetea hatua yake ya kumtuma Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga,kuzuru taifa la sudani kusini,ili kunusuru hali ya uwezakano wa kuzuka mapigano.Haya yanajiri baada ya kuibuka tetesi za kukamatwa kwa makamu wa rais wa kwanza wa taifa hilo Riek Machar,aliyedaiwa kuzuiliwa nyumbani kwake yeye pamoja na mkewe ambaye ni waziri wa usalama wa taifa hilo.

Naibu wa rais profesa Kithure Kindiki,amesema kuwa taifa la kenya limejitolea kuhakikisha kuwa linatoa msaada wake kwa mataifa yanayokumbwa na mizozo ili kulinda haki za kibinadamu.Aidha kwingineko kiongozi wa wiper kalonzo musyoka,ametilia shaka uwepo wa vikosi vya kenya katika taifa la Haiti akidai kuwa ni wakati serikali ya Kenya kuruhusu vikosi hivyo kurejea nchini baada ya kuripotiwa visa vya baadhi ya maafisa wa usalama kupoteza maisha yao na wengine kutoweka kwa njia tatanishi.