

By Emmanuel Wabomba, TMG journalist.
Waziri wa usalama wa ndani kipchumba Murkomen amefika leo mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama ili kuuelezea hali ya usalama wa taifa.
Murkomen alitaka kamati hiyo kupendekeza mgao zaidi kwenye kitengo cha DCI ili kufanikisha utendakazi wa tume licha ya wakenya kusubiri kwa muda kupata haki baada ya kitengo hicho kuanza uchunguzi.Waziri huyo alikiri kuwa kaunti ya Trans Nzoia ina genge la vijana wanaotumiwa na baadhi ya wanasiasa kuzua vurugu kwenye hafla mbalimbali za umma.
Aidha alitoa onyo kwa viongozi wanaoendesha semi za uchochezi huku akisema kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.Licha ya hayo,seneta wa kaunti ya Nandi Samson cherargei anaendelea kusisitiza kuwa ni lazima rais William Ruto aongoze mihula miwili licha ya upinzani kutoka kwa baadhi ya viongozi na wananchi.

Hatua inayoonekana kuwa kampeni ya mapema takribani miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.Cherargei ametishia kuwasilisha tena bungeni mswada kwamba muhula wa rais kuhudumu uongezweโhatua inayoonekana kuendelea kuchochea kupanda kwa joto la kisiasa nchini Kenya.