
Deputy President of Kenya, Rigathi Gachagua, gestures as he addresses the media during a press conference at his official residence in Nairobi, on October 7, 2024, ahead of the National Assembly vote on his impeachment motion. The 59-year-old deputy to President William Ruto is accused of corruption, undermining the government and practising ethnically divisive politics, among a host of other charges. (Photo by LUIS TATO / AFP) (Photo by LUIS TATO/AFP via Getty Images)

By Felix Wanjala .
Hisia mseto zinazidi kutolewa kuhusu muungano mpya wa upinzani unaopaniwa kuundwa ili kumenyana na rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.
Baadhi ya wananchi wanawataka viongozi wa upinzani kushirikiana kwa pamoja ili kuafikia malengo hayo.Aidha baadhi ya wananchi wanampendekeza aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani kwenye serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta,Daktari Fred Matiang’i, kupewa tiketi ya kupeperusha bendera ya Urais kwenye uchaguzi ujao.
Wakaazi hao wamemsuta rais William Ruto kwa madai kwamba aliwafeli wakenya baada ya kushindwa kutimiza Baadhi ya ahadi alizotoa wakati wa kampeni zake.Hata hivyo,baadhi yao walipuzilia mbali juhudi za muungano huo, wakidai kuwa vigogo wake walikuwa maafisa wakuu serikalini na walishindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Hapo jana, viongozi wa upinzani walikutana nyumbani kwake aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua katika eneo la wamunyoro eneo bunge la Mathira kaunti ya nyeri na hapa waliahidi kufanyia kazi pamoja.
Waziri wa zamani Fred Matiang’i aliahidi kuwa iwapo atateuliwa kupeperusha bendera na kuchaguliwa kama rais, atahakikisha amerejesha imani ya wakenya dhidi ya serikali.Viongozi hao pia walitoa onyo kwa baadhi ya viongozi waliodai wanamshambulia rais mstaafu Uhuru Kenyatta kutokana na matamshi yake kwamba vijana wajitokeze kupigania haki zao.