
Legal or auction gavel flat design illustration concept.

By Felix Wanjala.
Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kwamba Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu hakufaa kuunda jopo la majaji lililosikiliza kesi ya kumwondoa mamlakani aliyekuwa Naibu wa Rais, Rigathi Gachagua, umeibua maoni tofauti kutoka kwa viongozi wa kisiasa.
Viongozi wa upinzani sasa wanamtaka Naibu wa Rais wa sasa, Profesa Kithure Kindiki, kujiuzulu, wakisisitiza kuwa Rigathi Gachagua ndiye anayestahili kushikilia wadhifa huo kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya, Ibara ya 146(2)(b), nafasi ya Naibu wa Rais inaweza kuwa wazi endapo atafariki, atajiuzulu, au atabanduliwa kwa mujibu wa sheria.
Iwapo nafasi hiyo itakuwa wazi, rais anao wajibu wa kumteua mtu mwingine kushikilia nafasi hiyo, kwa idhini ya Bunge la Kitaifa. Katika mchakato huo, rais atapendekeza jina la mgombea mmoja ambalo litatumwa bungeni kwa uchunguzi na uidhinishaji.
Endapo atapitishwa, atakula kiapo na kuanza rasmi majukumu ya Naibu wa Rais.Akizungumza katika eneo la Juja hapo jana, Rigathi Gachagua alisisitiza kuwa ana imani na idara ya mahakama, akieleza kuwa anaamini Wakenya wataendelea kupata haki kupitia idara hiyo.
Excellent ึoods from you, man. ำ’ve understand yoแฅr stuff
โฒฃrevious tแง and you are just extremely
fantastic. ำ actualโ ผy like whษt you have acquired าปere, certainl๏ฝ like whะฐt yoีฝ’r๏ฝ saying and the way in whicาป าฏou ัay it.
Yoแฅ maาe it entertaining ษnd yฮฟu still care fแงr to keep it wise.
I can’t wait to ะณead mแฅch moะณe from you. ฮคhis is really a wonderful website.
Here is my blog :: bclub com
I am in fact thankful to the owner of this website who has shared this fantastic piece of writing at
here.