
Flag of Kenya and location on world map

By Felix Wanjala.
Katika maadhimisho ya sherehe za Madaraka Dei ya 62, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Raila Odinga, kaunti ya Homa Bay, Rais William Ruto aliwaongoza viongozi wengine kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya wakati Kenya ilipopata mamlaka ya kujitawala kutoka kwa serikali ya kikoloni ya Uingereza mnamo Juni 1, 1963.
Katika hotuba yake, Rais Ruto aliwakosoa vikali wapinzani wake waliokuwa wakiendeleza kauli ya _”One term,”_ akiwataka kutafuta ajenda mbadala badala ya kuikosoa serikali yake, akisisitiza kwamba utawala wa Kenya Kwanza utaendelea kutekeleza maendeleo _”bila break.”_Kiongozi wa ODM, Raila Odinga, katika sherehe hizo, alimwambia Rais Ruto kwamba msamaha wake kwa vijana wa Gen Z hautoshi.

Alihimiza serikali kuanza kutoa fidia kwa familia zilizopoteza wapendwa wao pamoja na waliojeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.Viongozi hao walitetea ushirikiano wao, wakisema kuwa kubuni Serikali ya Mapana ilikuwa hatua ya kuunganisha taifa bila kuegemea upande wowote.
Aidha, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga alisisitiza msimamo wake kwamba baadhi ya majukumu yanayofanywa na wabunge, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa mgao wa fedha za basari ( _NG-CDF_), yapewe magavana ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Katika hotuba yake, Rais Ruto aliangazia sekta zilizopewa kipao mbele na serikali yake, ikiwa ni pamoja na:Ujenzi wa nyumba za bei nafuu,Mageuzi katika sekta ya afya akiwataka Wakenya kujisajili na bima mpya ya SHA,Elimu ambapo alisifia mfumo mpya wa ulipaji karo katika vyuo vikuu licha ya kupingwa na wadau mbalimbali,Kilimo, akiahidi kuendelea kufanya mabadiliko ili kuinua wakulima.
Maadhimisho hayo yalihitimishwa kwa wito wa umoja na maendeleo kwa taifa.