

BY ALEX WEKESA.
Mbunge wa Kanduyi John Makali ametoa changamoto kwa serikali ya kaunti ya Bungoma kushirikiana na ofisi yake ya NG-CDF ili kununua shamba litakalosaidia katika upanuzi wa chuo cha wanafunzi wanaosomea kozi mbalimbali za Matibabu (KMTC) tawi la Bungoma.
Katika hotuba yake wakati wa ibada ya mazishi ya Juliana Osyanju mjini Bungoma Makali amesema tayari chuo hicho kina hekari mbili ya shamba pekee ,suala analolisema kutokana na kuongeza kwa idadi ya wanafunzi wanaozidi kujiunga na chuo hicho,pana haja ya chuo kuongezewa hekari zingine za shamba ili kuruhusu chuo hicho kujiendeleza .
Mbunge huyo wa Ford_Kenya Kenya ambaye ameongoza eneo bunge la Kanduyi kwa muhula wake wa kwanza na kutarajia kuchaguliwa tena mwaka wa 2027, amesema kupitia katika bajeti yake ya kipindi cha kifedha cha 2025/2026 ametenga takribani KSh 10 Million pesa zitazosaidia kupiga jeki chuo hicho kujinunulia shamba zaidi.
Kadhalika, Makali amefichua kwamba mpango upo wa kuwawezesha baadhi ya wanachama wa bodaboda kutoka eneo zima la Kanduyi kujiunga na chuo hicho ha matibabu ili kuwapa fursa ya kupata ujuzi unaofungamana na masuala ya matibabu ili kujikimu katika maisha yao ya baadae.Mbunge Makali alimshukuru rais William Ruto kwa kuitikia ombi lao la kupandisha hadhi hospitali ya rufaa ya Bungoma hadi kiwango cha Sita.”Bwana rais tunashukuru kwa kutukumbuka,watu wetu watapata matibabu ya karibu, hawatalazimika kusafiri mwendo hadi kaunti zingine kutibiwa magonjwa sugu kama vile kansa”, Makali alisema.

Hospitali ya kiwango cha sita (level 6) ni taasisi ya afya yenye majukumu muhimu katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii. Majukumu yake kwa ujumla ni pamoja na:Kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa mbalimbali, ikiwemo upasuaji wa ngazi ya juu, utunzaji wa wagonjwa wenye magonjwa sugu, na huduma za dharura.Kutoa huduma za afya ya akili na msaada kwa wagonjwa wenye matatizo ya kiakili.Kutoa matibabu na huduma kwa wagonjwa wenye majeraha makubwa na matatizo ya mifupa.
Kutolewa kwa mafunzo na elimu kwa wahudumu wa afya, ikiwa ni pamoja na madaktari na nesi.Kushiriki katika utafiti wa kisayansi ili kuboresha huduma za afya na kutatua matatizo yanayohusiana na magonjwa.Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu lishe, magonjwa na jinsi ya kujikinga, na kuhamasisha huduma za afya miongoni mwa zinginezo.