

Tunaanzia pale kwenye jumba la kifahari la Don Julio(Bana yake Ramon) huku Olga,dada yake Ramon,akimwambia Don Julio kuwa kumtorosha Ramon kutoka gerezani ilikuwa ni idea mbaya sana kwa sababu polisi wataanza kuwatilia Mashaka na inaweza kuharibia biashara Yao soko.
Don Julio anamwambia Olga kwamba atalishughulikia Hilo jambo asiwe na wasiwasi. Don Julio anamtukana olga kwa kutokuwa na uaminifu kwake. Kwa kawaida sote tunafahamu kuwa Don Julio anampenda sana Ramon kumliko Olga japokuwa wote ni wanawe(watoto wake). Olga siku zote hajawai kumpenda Ramon.Huku Nako Tindeng anaambiwa na Noy kwamba wamjuze Tanggol ukweli kuhusu uhalisia wake. Tindeng(Mama yake Marites)— kwa ufupi Tindeng ni bibi yake Tanggol. Tindeng anakataa kwamba wakimwambia Tanggol ukweli watavunja familia Yao pamoja na furaha Yao yote kabisaaa.
Rigor anasisitiza kwa Marites kwamba aongee na Tanggol kwa sababu yeye subira yake inaisha kabisa. Rigor Yaani anchukia Tanggol wetu sanaaa jameni. Marites anakubali kwamba ataongea na Mwanawe. Marites ni make mwenye heshima kubwa sana na ni mnyenyekevu kwa sababu siku zote hapendi malumbano Kati yake na mumewe Rigor.

Tanggol ili kurekebisha makosa kwa babake Rigor,anaamka mapema na kuunda kiamsha kinywa ili familia yake ile Lakini babake anakataa katakata kwa kusema kwamba yeye ameshiba na kumbuka ni asubuhi hiyo. David anafurahia sana kwa kuwa Baba yake hampendi Tanggol. Marites anamwambia Tanggol kwamba aepukane na utundu pamoja na mambo mabaya kwa kuwa anamfunza kaka yake Santino tabia mbaya.
Tanggol pia alitoroka na kuacha shule msisahau.Makosaaa….nawaambia this week ndo Kuna Mambo motooo ndani ya Gangs Of Manila kwenye runinga ya mwananchi ya Tandao TV. Habari sasa ya Ramon kutoroka jela imefika kwenye runinga za kimataifa. Marites anaona hizo taarifa huku anapatwa na kiwewe kwa kuwa Ramon alisema atamrudia mtoto wake. Marites analia huku akimwambia mama yake Tindeng na Noy.
Pia Boss ama maarufu Don Julio anaona hiyo taarifa kwenye runinga akiwa na Olga. Olga Bado tu ana hofu huku Ramon anamtishia Olga kwamba akijaribu kumsaliti atamuua haraka sana kwa kuwa anamjua. Ramon hapendi usaliti hata kidogo. Inspekta wa polisi anakuja haraka na jeshi la polisi kwenye nyumba ya Don Julio kumtafuta Ramon Lakini Don Julio anakana kwamba hajaskia hata hizo habari hata kidogo. Olga anaandaa kifurushi Cha pesa nyingi sana ili kumpatia afisa huyo wa polisi kama hongo ya kunyamazia hiyo kesi.
Tanggol na genge lake watoka kwenda missions za kupora watu kwa streets Tena huku wakiwa wamevaa vizuriiii sana ndo watu wa kawaida wasiwashuku hata kidogo.Sasa kwa wale ambao wanashangaa kwa Nini jina la kipindi Chetu ni Gangs Of Manila,hapa sababu ndio hii; Kwenye Episode ya Leo kutadhihirika waziwazi kwamba Kuna magenge sufufu Kwenye mji wa Manila hasahasa kutoka kwenye mji mdogo wa Quiapo. Leo mtapata fursa kinda kindaki ya kuona jinsi Tanggol (Cardio Dalisay) na genge lake watakavyowaibia watu kwenye mji.Leo Kuna BURUDANI kemkem kwani Tanggol naenda kumuibia Supremo(Mhusika anayeingia Leo ambaye alikuwa rafiki mkubwa sana wa cardo kwenye Brothers), Tanggol anaenda kumuibia Supremo Kisha inageuka baadae kuwa kwamba Supremo ndiye ambaye amewaibia wao. …inaitwa turning the tables.
Leo pia Kuna mhusika wenu mpendwa sana kutoka kwenye telenovela ya kimataifa ya Wildflower anaingia kwenye kipindi kama Greg. Greg ni mtoto wa Olga. Sasa Greg anamuita Ramon kuwa mjomba wake. Greg Ako na hasira za haraka sana. Tutapata fursa ya kutazama wahusika wakuu sana kwenye sanaa ya uigizaji kutoka Ufilipino.Pia nataka niwaeleze kwamba kwenye kituo Cha polisi tunao Hawa polisi ambao ni main characters; kunaye Rigor Dimagba,baba yake David,Santino na baba mlezi wa Tanggol na mume wa Marites,tunaye Afisa Mando, rafiki wa kiume na partner wa Rigor, tunaye Afisa Lena Cortez utaona kwenye badge yake kumeandikwa Cortez L. Lena anakuwaga anampenda Rigor sana lakini hataki kumwambia.
Usikose kutazama kipindi hiki Kila siku ya wiki (Jumatatu hadi Ijumaa) saa mbili kamili za usiku kwenye runinga ya Tandao. Leo Vitu ni murwa sana na Kuna wahusika wakuu wengi sana ambao tutaweza kuwaona kuanzia hapo Kesho na tutajadili kuwahusu hapa kwenye kurasa wetu wa Fesibuku Tandao Tv Kenya.