
FILE-Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang'ula kwenye hafla fulani.PHOTO/TANDAO MEDIA/FILE

BY FELIX WANJALA.
Mvutano wa Uongozi ndani ya Ford Kenya: Majimbo Kalasinga dhidi ya Moses Wetang’ula.
Joto la kisiasa katika chama cha Ford Kenya,lilianza na onyo, kutoka kwa kiongozi wa chama Moses Wetangula,akimtaka mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga, kuwa na heshima kwa chama hicho.Matamshi ya Wetangula yalionekana kumkera Kalasinga,aliyetaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi kwa kuhofia usalama wake.
Kutia msumari moto kwenye kidonda,wandani wa wetangula wanamtaka Kalasinga kuwa na heshima kwa chama cha Ford Kenya ikinzingatiwa kuwa yeye ni mwanachama.Na baada ya kuapa kuwa anakukujia chama cha ford Kenya anaonekana kukumbana na upinzani mkali

Safari ya kunyakua chama hicho ikianza,Majimbo anahitajika kutafuta uungwaji mkono zaidi kutoka kwa wananchi,ila baadhi wanaonekana kutofautiana naye katika hatua hiyo.Chama cha Ford Kenya kimeongozwa na viongozi wanne katika safari yake ya kisiasa
- Jaramogi Oginga Odinga – alikuwa kiongozi wa FORD-Kenya 1992
- Michael Kijana Wamalwa – alichukua nafasi baada ya kifo cha Odinga mwaka 1994.
- Musikari Kombo – baada ya Wamalwa kufariki mwaka 2003.
- Moses Wetang’ula – aliingia uongozi rasmi mwaka 2011 na ameendelea kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa chama hicho.