
BY FELIX WANJALA
Mgombea wa ugavana Kaunti ya Bungoma Timothy Wanyonyi,amefanya mkutano na washikadau mbalimbali wa afya kwenye Kaunti ya Bungoma,katika makao yake ya mikakati ya Eninga eneo bunge la Kanduyi.
Maafisa hao wa afya waliapa kumuunga mkono kiongozi huyo kuchaguliwa kama Gavana katika uchaguzi mkuu wa 2027.Baadhi walitoa wito kwa mgombea huyo kuzingatia swala la kupandishwa mamlaka kwa wahudumu wa afya ambao wamehudumu kwa mda mrefu pamoja na kuzingatia swala la kuajiri wauguzi kwa mkataba wa kudumu.Aidha Wanyonyi ameapa kuzingatia maslahi ya wahudumu hao wa afya ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wakaazi wa Kaunti ya Bungoma.
Kati ya maswala kiongozi huyo aliapa kutekeleza ni kushughulikia swala la uajiri wa wauguzi kwa mkataba wa kudumu,Kuzingatia upandishwaji wa vyeo,Kutetea maslahi yao katika ngazi ya kitaifa,kuipa sekta ya afya uhuru wa kuhudumu pamoja na kuanzisha swala la mishahara ya wauguzi.