Akiwaongoza wahudumu wa nyanjani kwenye mkutano wa kuimarisha afya katika kaunti ya Trans nzoia, mwakilishi wadi wa Kiminini Joshua Amwai aliangazia changamoto za kiafya zinazowakumba wakazi wa eneo hilo na namna ya kuzitatua.
Kupitia Emma Mabeya ambaye ni mhudumu wa afya nyanjani CHP, ilibainishwa kuwa wakazi wengi huchelewa kupata matibabu kwa kukosa ufahamu na kuchelewa kugundua magonjwa hayo.
Serikali ya kaunti ya Trans nzoia iliahidi kushirikiana na wahudumu wa afya nyanjani ili kuhakikisha wakazi wale wamefanikiwa kupata ufahamu wa matibabu hasa walio na ulemavu.Walizidi kuwahumiza wakazi wa kaunti hii hasa wa mashinani kufahamisha serikali changamoto zao ili mikakati mkabala iwekwe.
Baadhi ya changamoto za kiafya zinazowakumba wakazi hasa wa mashinani ni ukosefu wa ufahamu wa matibabu, kutomudu ada ya matibabu, kuchelewa kugundua magonjwa, kutekeleza mahitaji ya wanajamii walemavu na uhaba wa vifaa vya matibabu.
Abigaely Wanjala