

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula, amezungumza kuhusu uhusiano wa rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga,iwapo unabusiana na madai ya kubanduliwa kwake mamlakani,aidha wetangula anadai ushirikiano baina ya viongozi hao ni wa kuleta umoja wa taifa.Kinyume na Wetangula,wakaazi mjini Bungoma waliandaa maandamano hapo jana, wakidai kuwa huenda ushirikiano wa rais na kiongozi wa upinzani, ndio chanzo cha masaibu yanayokumba kiongozi wa chama cha Ford Kenya.

Aidha spika wetangula,anasema jukumu lao kama viongozi,ni kuhakikisha wakenya wanaishi kwa amani na kila eneo linanufaika na maendeleo.Kwa upande mwingine rais William Ruto akiongoza kongamano kuhusu kawi salama jijini Nairoi,alitaja ushirikiano miongoni mwa viongozi,kama njia pekee itakayofanikisha maendeleo.Aidha rais Ruto, alizungumzia ziara yake ya hivi majuzi kaskazini mashariki mwa taifa,ambapo aliahidi wenyeji ujenzi wa baadhi ya barabara, Wakenya mitandaoni wamekuwa wakifanyia utani ahadi alizotoa wakati wa ziara hiyo.Rais ameahidi serikali yake itatimiza ahadi hiyo kwa wananchi wa kaskazini mashariki mwa taifa, kinyume na dhana kutoka kwa wapinzani wake kwamba huenda ilikuwa ni ahadi hewa.