

BY EMMANUEL WABOMBA,TMG JOURNALIST.
Ni majibizano yanayoshuhudiwa baina ya msaidizi wa rais Farouk Kibet na gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya.Kibet anamshtumu Natembeya kwa madai ya kuendelea kuhujumu utendekazi wa serikali ya rais William Ruto.
Madai haya ya Farouk yalipingwa vikali sana na Natembeya aliyemtaka msaidizi huyo wa rais,kupeana nafasi kwa viongozi wa upinzani kuikosoa serikali iwapo inafeli katika utendekazi wake.Natembeya alitilia shaka utendekazi wa msaidizi wa Rais akidai kuwa nia yao kama serikali ni kutaka kulemaza juhudi za upinzani kumtetea mwananchi wa kawaida.

Na je Farouk Kibet ni nani,mara kwa mara ameonekana akiandamana na rais William Ruto katika hafla tofauti za umma,ila kwa wakati mmoja baadhi ya viongozi wakuu serikalini walionekana kuweka wazi majukumu yake ndani ya serikali.Baadhi walimtaja kuwa kiongozi mchapa kazi na asiye na afisi maalumu.
Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua amewahi kumtaja Farouk Kibet kama kiungo muhimu katika kuratibu siasa za muungano wa Kenya kwanza iliyopelekea wao kupata ushindi dhidi ya wapinzani wao.Kwa upande mwingine gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya,Mnamo Juni 2019, aliteuliwa kuwa Kamishna wa Mkoa wa Bonde la Ufa.
Katika kipindi chote cha utumishi wake kama Kamishna wa Mkoa, alionekana kuchukua msimamo mkali wakati huo akijaribu kurejesha amani katika eneo la Bonde la ufa.Natembeya aliamua kujiingiza katika siasa;uamuzi ulioleta mabadiliko makubwa, baada ya kujiuzulu kutoka wadhifa wake kama Kamishna wa Mkoa mnamo Januari 2022 ili kugombea kiti cha Ugavana.
Baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022, Natembeya alichaguliwa kuwa Gavana wa Kaunti ya Trans-Nzoia na ameonekana kuwa mkosoaji mkuu wa serikali ya Rais William Ruto.
