BY SYPHROSE NAFULA

🔴Viongozi wa Serikali Wapiga Marufuku Siasa za Ukabila, Wasisitiza Umuhimu wa Umoja.
Baadhi ya viongozi wa serikali wamelaani vikali siasa za ukabila wakidai zinatishia umoja wa kitaifa. Akizungumza wakati wa hafla ya uchangishaji fedha kwa vikundi vya wanawake katika Kimilili Constituency, Farouk Kibet aliwakosoa aliyekuwa Rais na viongozi wa upinzani kwa madai ya kutumia mgawanyiko wa kikabila kujipatia umaarufu kisiasa. “Baadhi ya viongozi wanatumia siasa za ukabila badala ya kuleta ajenda za maendeleo zinazowanufaisha wananchi,” alisema Kibet.
Aliwahimiza Wakenya kuunga mkono viongozi wanaotangaza amani na mshikamano.Gavana wa Bungoma, Ken Lusaka, naye alisema serikali imejitolea kufanya kazi na viongozi wote bila kujali tofauti za kisiasa ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inafika kwa kila raia.”Maendeleo ya wananchi yanapaswa kuwa kipaumbele chetu kuliko siasa za kutugawanya,” aliongeza Lusaka.Mbunge John Bwire pia aliwataka viongozi kutumia majukwaa yao kuunganisha Wakenya badala ya kuwatenganisha. “Kazi yetu ni kujenga taifa moja, sio kulirega kwa misingi ya ukabila,” alisema.

Hafla hiyo ililenga kuwainua kiuchumi vikundi vya kina mama kupitia michango iliyokusanywa. Viongozi walisisitiza kuwawezesha wanawake ni njia moja muhimu ya kukuza uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.Wakati taifa likiendelea kujadiliana kuhusu siasa, wito wa viongozi hawa ni mmoja: Acha migawanyiko, tushikamane kwa maendeleo.