A drug addict uses a syringe to inject a narcotic into his arm as others smoke cocaine-infused marijuana at a field in Dagoretti in Nairobi county on January 19, 2024. A five-year national survey published in 2022 by the National Survey on the Status of Drugs and Substance Use in Kenya found that one in every 6 Kenyans aged 15 65 years are currently using at least one drug or substance of abuse ranging from tobacco, alcohol, khat, cannabis, prescription drugs, cocaine and heroin. (Photo by Tony KARUMBA / AFP) (Photo by TONY KARUMBA/AFP via Getty Images)
BY SIMIYU VIONA

Tatizo la matumizi ya dawa za kulevya nchini linaendelea kuibua hofu kubwa, hasa katika eneo la Kabuchai, huku vijana wengi wakipoteza mustakabali wao kutokana na uraibu unaochangia ongezeko la uhalifu, umaskini, na kuvunjika kwa familia. Serikali pamoja na wadau mbalimbali wanahimizwa kushirikiana kwa karibu katika kukabiliana na changamoto hii inayohatarisha kizazi kijacho.Katika hafla ya kumuapisha Naibu Chifu wa kijiji cha Khachonge, Katibu Mkuu wa Idara ya Utawala wa Ndani, Beverly Opwora, aliwataka wananchi, viongozi wa kijamii na vyombo vya usalama kushirikiana kikamilifu ili kufanikisha vita dhidi ya dawa za kulevya.
Opwora alisisitiza kuwa wazazi wanapaswa kuwafuatilia na kuwaelekeza vijana mapema ili kuzuia uraibu wa mihadarati.“Matumizi ya dawa za kulevya yanaathiri maendeleo ya jamii hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa,” alisema Opwora, akiongeza kuwa serikali imeweka mikakati madhubuti kudhibiti biashara ya mihadarati na pombe haramu katika maeneo yote nchini.Katibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Juma Mukwana, aliwataka vijana kujiepusha na makundi mabaya yanayojihusisha na dawa za kulevya na badala yake kujikita katika shughuli za maendeleo, biashara ndogo ndogo, na kilimo ili kujijengea maisha bora.
Alisema serikali inaendelea kuimarisha programu za uwezeshaji wa vijana kiuchumi ili kupunguza utegemezi na ukosefu wa ajira unaochochea uraibu.Aidha, Mukwana alisisitiza kuwa maendeleo ya taifa hayawezi kupatikana endapo vijana wataendelea kuangamizwa na dawa za kulevya. Alihimiza viongozi wa dini, walimu, na mashirika ya kijamii kuendelea kutoa elimu na ushauri kwa vijana kuhusu madhara ya mihadarati.Viongozi hao pia waliwataka maafisa wa usalama kuongeza doria na uchunguzi dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wanaolenga vijana shuleni na maeneo ya biashara.

Serikali imeongeza maafisa wa kitengo cha kupambana na mihadarati na kuendesha operesheni mbalimbali za kukabiliana na changamoto hiyo.Wakazi wa Kabuchai wameitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wasambazaji wa dawa za kulevya kwani familia nyingi zimeathirika na baadhi ya vijana kushindwa kuendelea na masomo kutokana na uraibu.Hafla hiyo, pamoja na kumuapisha naibu chifu wa Khachonge, ilitumika kama jukwaa la kuhamasisha mshikamano wa jamii katika kupambana na changamoto zinazowakumba vijana. Viongozi walisisitiza kuwa mapambano dhidi ya mihadarati yanahitaji mshikamano wa kila mwananchi ili kuhakikisha kizazi kijacho kinaishi katika mazingira salama na yenye matumaini.
Matumizi ya Dawa za Kulevya Yazua tahadhari na mshuko Kabuchai