Viongozi wa Azimio, huku wakiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa Kwa Aburu Odinga, wamekashifu maongezi ya Rais Ruto wakati alipokuwa Kwa ziara ya siku nne kwenye mkoa wa Nyanza.
Kinara wa Azimio, Raila Odinga, amemsifu Kalonzo Kwa uaminifu wake na kisha akasema Kuwa Kalonzo yu mara kumi zaidi ya Ruto.
” Kalonzo ameshinda bwana Ruto mara kumi”
Raila Odinga amesisitiza kuwa, atasimama kidete na Kalonzo Musyoka.Viongozi wa Azimio wamewataka wakamba na wajaluo kuendelea Kuwa na umoja waliokuwa nao wakati wa Kura.
Hata hivyo, viongozi wa ukambani wanamatumaini Kuwa wajaluo watawaunga mkono .Paul Simiyu ambaye ni mkaazi wa Bungoma amesema Kuwa licha ya Raila kupigania wananchi wa chini, amefanya vyema kumuunga mkono Kalonzo ambaye ataleta mafanikio kwenye chama.
Kinara wa Azimio Raila Odinga, Leo amepuuzilia mbali Ripoti ya kumpendekeza Kalonzo Musyoka .
Kupitia Kwa msemaji wake Dennis Onyango, Raila amesema Kuwa kumsifu kwake Kwa Kalonzo happy jana hakufai kuchukuliwa Kuwa msimamo wa muungano wa Azimio kumuidhinisha Kalonzo Kuwa mwaniaji wake wa Urais.
Raila pia amesema Kuwa muungano utatoa nafasi Sawa Kwa waniaji wa kiti hicho na tangazo hilo litatolewa mwaka moja kabla ya uchaguzi wa elfu mbili ishirini na Saba.
Magret Ongwala