Ni katika shule ya msingi ya Akriamet wadi ya Angurai kaskazini kaunti ya Busia ambapo wanafunzi watatu wa kike hawajahudhuria maombi yaliyoandaliwa kwa watahiniwa wa darasa la nane,mmoja akiwa mjamzito wengine wawili wakiwa wamejifungua siku chache zilizopita.
Baadhi ya walimu katika shule hii wamefichua kuwa,wakati mwingine wanalazimika kufunga safari kuwatafuta wanafunzi kutoka nyumbani mwao ambapo baadhi ya wazazi wanalaumiwa kwa kuwapuuza wana wao.
Katika shule ya msingi ya Osieko wadi ya Bunyala Kusini eneo bunge la Budalangi kaunti ya Busia,kwenye mpaka wa kaunti za Busia na Siaya mita chache kutoka ziwa Victoria,baadhi ya wanafunzi hapa hujipata na majukumu ya uzazi mapema.
Kukosekana kwa uhamasisho wa kutosha kuhusu masuala ya hedhi na dhana potovu,zinasababisha wasichana wengine kujipata kwenye mtego na baadae kupachikwa mimba.
Na Elizabeth Kisiangani