Wakulima kwenye Kaunti ya SIAYA wameshauriwa kupanda mmea tofauti kwenye Mashamba yao ili kuongeza mapato yao.
Waziri wa kilimo kaunti ya Saya Silvester Kokoth, akizungumza kwenye sherehe za kuadhimisha siku ya chakula duniani, amesema Kuwa idara yake inafanya kila iwezavyo ili kuwavutia vijana kukumbatia kilimo kuhakikisha Kuwa kaunti hiyo ina chakula cha kutosha.
Waziri huyo amesema Kuwa iwapo wakulima kwenye Kaunti hiyo ya SIAYA watakumbatia ukulima wa vyakula kama mhogo, members, viazi tamu na ndizi kaunti hiyo itakuwa na uwezo wa kuwaajiri vijana .
Hata hivyo, Mkurugenzi wa kilimo Isaac Munyendo kutoka Kaunti ya Saya, amewataka vijana wasomi kukumbatia kilimo cha samaki na pia matunda ili kuzuia ukosefu wa ajira kwenye Kaunti hiyo .
Na Magret Ongwala