Wakizumgumza katika hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake mashinanib, wanawake walinufaika na
msaada kutoka shirika la Groots Kenya.
Miradi kutoka Groots Kenya ni kama uongozi,ukulima na biashara ,ilitajwa kama njia mwafaka ya
kuwakwamua wanawake hawa kutoka Umaskini na utegemezi. Hata hivyo shirika hilo linapatikana
katika kaunti mbili tuu za kitui na Laikipia.
Naibu Gavana wa kaunti ya Laikipia Ruben Kamaru alisisitizia umuhimu wa wanawake kuwa imara katika
jamii na suala hili husaidia katika shida kama za ukosefu wa chakula.Alizidi kutaja miradi kama ya
mashimo ya maji miongoni mwa miradi ingine ambayo wanawake wamehusishwa kwa kamati hizo.
Aisha shida ambazo wanawake wa mashinani hukumbana nazo ni kama unaguzi wa jinsia, ukosefu wa
usalama, majukumu ya ulezi, kutopata ajira mbadala na upungufu wa fursa za elimu katika baadhi ya
maeneo.
Abigaely Wanjala