Sheria ya fedha iliyopitishwa mwezi Juni mwaka huu,ilianzisha mpango wa msamaha wa riba,adhabu na faini zilizotozwa juu ya ushuru kabla ya tarehe 31 Desemba mwaka jana.
Chini ya mpango huo,wakenya waliokamilisha malipo ya ushuru na kubakisha riba na faini watapata afueni moja kwa moja,walio na salio la ushuru watatuma maombi kupitia tuvuti ya mamlaka ya ukusanyaji ushuru ya i-tax na kupendekeza jinsi watakamilisha malipo kabla ya tarehe 30 mwaka ujao.
Wakizungumza mapema leo,maafisa wa mamlaka hiyo walitangaza kuwa shilingi bilioni 3.4 tayari zimekusanywa chini ya mpango huo unaolenga kukusanya shilingi bilioni hamsini kutoka kwa walipa ushuru milioni 2.8.
Mwezi uliopita,mamlaka ya KRA ilianza kuwatuma maafisa waliopokea mafunzo ya kijeshi,kuhakikisha sheria za ushuru zinafuatwa. Mamlaka hiyo sasa imesema kuwa itaunganisha mifumo yake ya malipo na ile ya kidigitali kama vile mpesa,ili kuhakikisha wafanyibiashara wa juakali wanalipa ushuru.
Walio na kesi za ushuru mahakamani,pia wameshauriwa kuziondoa na kuzitatua nche ya mahakama kabla ya tarehe 30 mwakani. Mamlaka ya KRA ikiongeza juhudi zake za kukusanya Ushuru ambao wamekuwa wakilalamikia kuongezeka kwa gharama ya maisha.
Na Elizabeth Kisiangani |