Tume ya mawakili nchini LSK ,ilibainisha kwa ripoti namna Brian Mwenda Njagi aliiba utambulisho wa
uwakili ambao ulikuwa wa Brian Mwenda Ntwiga wa jina sawa kama yeye.Tume hiyo ilitoa wito kwa
tume ya uchunguzi DCI kumchukulia hatua kali ya kisheria na kumkamata kwa makosa hayo.
Ilibainishwa kuwa, licha ya Mwenda kukosa vyeti vya uanasheria,alionyesha tajriba ya umahiri na ujasiri
akishughulikia kesi nyingi zikiwemo za hadhi ya juu. Kwa jumla Mwenda ameweza kushinda kesi ishirini
na sita tangu kuanza uanasheria.
Wadau mbalimbali na miungano ikiwemo muungano wa wafanyakazi nchini COTU na ule wa wanafunzi
wa vyuo vikuu KUSO, ulimtetea Mwenda huku wakitaka apewe msaada ambao utamsaidia kutumia
ndoto yake ya uanasheria kwani alionyesha uwezo wa kuwa wakili mkubwa nchini.
Mwenda alifikishwa mahakama jijini Nairobi kwa tuhuma hizi,ambapo alihojiwa na maafisa wa tume ya
DCI , baadaye aliweza kuwachiliwa kwa bondi ya shilingi laki moja na hakusomewa mashtaka yoyote.
Na Abigaely Wanjala