
Wazee wa Baraza la Wazee wa Jamii ya Bakhayo kutoka Kaunti ya Busia wamejitokeza kupinga jaribio
lolote la kubadilisha mipaka ya maeneo yanayopakana na Kaunti Ndogo za Teso Kaskazini, Teso ya Kati,
na Teso Kusini wakati wa kubuniwa kwa Kaunti ya Teso, ambayo imependekezwa na baadhi ya viongozi.

Wazee wa Baraza hilo, wakiongozwa na Mwenyekiti wao Linus Mbalu Magero, Frederick Dindi Ndubi, na
Benzua Okwara Mutoka, wamesisitiza kuwa hawatakubali mipaka ya maeneo Bunge ya Namable na
Matayos kubadilishwa na wametoa onyo kali kwa wale wanaotaka kufanya hivyo.
Baada ya mkutano wao katika soko la Lupida eneo la Bunge la Namable, wazee hao wamewaonya
wanasiasa dhidi ya kuchochea wanajamii za Iteso na Bakhayo, ambao wamesema wameishi kwa amani
kwa muda mrefu.
Mapendekezo yao yalikuwa kwa wanasiasa kuwacha uchochezi kwa wanajamii, jamii hizo kuendelea
kuishi kwa amani, wanajamii kutumia haki kupata mali zao,mizozo ya mipakani kukomeshwa na zaidi ya
yote wanajamii kudumisha amani maeneo hayo.
Na Abigaely Wanjalaย