Imebainika Kuwa wakulima wa kaunti ya trans-nzoia hupoteza zaidi ya shilingi bilioni nne nukta tano ya mahindi kwenye msimu wa mvuno wa mahindi .
Wakulima hao huvuna mazao yao baada ya kusubiri Kwa miezi kadhaa. Hata hivyo, bado tu wao hukumbwa na changamoto ya kuharibiwa Kwa mazao yao na mvua .
Imetambuliwa Kuwa wakulima wa kaunti ya trans-nzoia hupoteza zaidi ya bilioni nne nukta tano ya mahindi, hii ikiwa ni kutokana na mvua kubwa, njia mbaya ya kuhifadhi mazao yaona kisha ununuzi wa mahindi Kwa bei mbovu na mawakala katika eneo Hilo
Wakielimishwa na waziri wa biashara Sternly Kirai, amewataka wakulima kukumbatia mbinu ya kuhifadhi mahindi katika maghala yalioidhinishwa na wizara ya kilimo, chini ya mpango wa warehouse receipt system council
Waziri wa kilimo katika kaunti hiyo, amewaomba wakulima kutoyauza mahindi yao Kwa sababu tu Wana haraka ya kuyauza, ilawazingatie gharama ya mbegu na nguvu walizotumia kwenye ukulima huo.