Waziri wa Usalama wa ndani Kithure Kindiki amepuuzilia mbali hofu kwamba misheni ya Kenya nchini Haiti itaigharimu hazina ya kitaifa.Akizungumza katika kaunti ya Meru,Kindiki aliwataka wabunge kuepuka siasa katika swala hilo huku serikali ikijiandaa kutafuta idhini ya bunge Kwa operesheni hiyo wiki ijayo.
Baraza la usalama Lili idhinishwa tarehe mbili Octoba ili kudhibiti ghasia za magenge nchini Haiti.Wiki Jana mahakama kuu ilisitisha misheni hiyo baada ya mwanasiasa Ekuru Aokoth kuwasilisha Ombi la kupinga Kwa misingi wa ukiukaji wa katiba .
Kithure Kindiki amejitokeza kuwahakikisha wakenya kwamba mpango huo utahidhinishwa na Bunge wiki ijayo kama inavyo takiwa na kifungu cha Mia mbili arubaini cha katiba .
Pia ameweza kupuuzulia mbali hofu kwamba Kenya itabeba gharama ya kuwatuma maafisa hao.Licha ya misheni hiyo kuidhinishwa na umoja wa taifa itategemea ufadhili wa wadhamimi kwani sio misheni inayoongozwa na umoja wa mataifa.
Viongozi wa upinzani kutoka chama cha ODM waliwasihi wabunge kutohidhinisha misheni hiyo.Lakini Kindiki amewataka wabunge kuzingatia umuhimu wa misheni hiyo bila kuingiza siasa.
NA FAITH MISANYA