Wananchi watalazimika kukaza mshipi zaidi,kufuatia tangazo la mamlaka ya udhibiti wa kawi na mafuta ya petroli.
Ongezeko la bei za mafuta ya petroli ni kwa shilingi 5.72,dizeli kwa shilingi 4.48 na mafuta ya taa kwa shilingi 2.45 kwa kila lita kati ya October na Novemba.
Hii inamaanisha kuwa jijini Nairobi lita moja ya petroli ya super itauzwa kwa shilingi 217.36,dizeli kwa shilingi 205.47 huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa shilingi 205.06.
Micah Nyongesa mwanabodaboda katika maeneo ya Bungoma,alisisitiza kwa kusema kuwa kile kinachowatatiza kama wanabodaboda ni kupandishwa kwa mafuta,maana imekuwa hali ngumu kwao kupata wateja wanaosafiri,ambapo hii imefanya gharama ya maisha kuwa ngumu zaidi.
Bila ruzuku hiyo ya PDL,lita ya super petrol ingeongezeka kwa shilingi 8.79,dizeli kwa shilingi 16.12 ma mafuta ya taa kwa shilingi 12.05.
Stephen Echesa mkaazi wa bungoma ambaye ni mwanabodaboda pia alilalamikia hili swala la ongezekonla bei ya mafuta ,ambapo anamuomba rais aweze kuwaangazia na kupunguza gharama ya maisha,ma ana ni changamoto kwao,kama wafanyibiashara wa bodaboda.
Elizabeth Kisiangani |