Rais William Ruto anatarajiwa kuidhinisha miswada minne ya afya na kuwa sheria siku ya Alhamisi, kabla ya maadhimisho ya siku ya mashujaa ambayo mada yake ni afya bora Kwa wote.
Katika shule ya pili ya kongamano la UHC, wadau wa afya wameangazia mno uhitaji wa dharura wa mfumo wa dijitali katika kutoa huduma za afya, ili kutokomeza changamoto za matumizi ya karatasi katika huduma za afya
Katika hatua ya kuimarisha utoaji huduma za afya nchini Kenya; mufumo wa dijitali inatarajiwa kurahisisha uwasilishaji wa takrimu mikakati ya rufaa katika hospitali na kuhakikisha rekodi za wagonjwa zinapatikana kwa urahisi katika vituo vyote vya afya.
Gavana wa Elgeiyo Marakwet Wesley Rotich ambaye alihudhuria Makutano huko aliangazia changamoto ambazo huenda zikakabili mufumo wa dijitali huku akipendekeza suluhisho.
Katika mpango wa ufanikishaji wa huduma ya afya Kwa wote ,Rais William Ruto anatarajiwa kuidhinisha miswada minne ya afya kufikia Alhamisi wiki hii na kuwa sheria .
Miswada hizo ni ;Mswada wa fedha za kustawisha vituo vya afya, mswada wa kujumuisha mfumo wa dijitali katika afya, mswada wa bima ya afya ya jamii na mswada wa huduma ya afya ya misingi.
Na Faith Misanya